Image
Image

MWANAFUNZI afa baada ya kuangukiwa na ukuta mkoani Ruvuma

MWANAFUNZI wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Seminari ya Muhuwesi, Tunduru mkoani Ruvuma, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta.
Mwanafunzi huyo alikumbwa na mkasa huo akiwa na wanafunzi wenzake ambao walikuwa wameweka kambi katika shamba la shule hiyo kwa ajili ya kuvuna mpunga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zubery Mwombeji, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
Kamanda Mwombeji alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Christian Liweta (15), na kwamba tukio hilo lilitokea katika mashamba ya shule hiyo yaliyopo katika kitongoji cha Maluluma, wilayani humo.
Alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi, saa saba usiku na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukuta wa jengo hilo kuliwa na maji yaliyokuwa yamefurika wakati wa mvua zilizonyesha msimu huu.
Kutokana na tukio hilo, Kamanda Mwombeji amewataka wananchi kuwa makini na matukio hayo, pindi wanapokwenda katika mashamba yao kuchungunza kwanza majengo yao kabla ya kuingia na kulala hasa wakati huu wa mavuno.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment