MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo
ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa
mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila inatarajia kutoa
hukumu Mei 17, mwaka huu.
Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi
hiyo mjini Kigoma, Ferdinand Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu
tarehe hiyo baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo
yao.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba
kupatiwa muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa
mahakamani hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Aliyekuwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa
uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo.
Katika
kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue
matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM, Hasna Mwilima badala
yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo.
Walalamikiwa
katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Hasna, aliyekuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa
msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali ambaye
anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Katika kesi hiyo, Wakili
Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku Kafulila akitetewa na mawakili
watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Rumenyela.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment