YANGA imetinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, lakini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm ametoa ya moyoni baada ya kusema kuwa timu hiyo imepata mafanikio hayo kutokana na mkwanja wa bosi wao, Yusuf Manji.
Pluijm ametamka kwamba juhudi kubwa zinazoonyeshwa na wachezaji wote wa Yanga akiwemo Donald Ngoma, Amissi Tambwe ambao wanatisha zaidi kwa ufungaji ni kutokana na mkwanja wa maana wanaopewa na tajiri huyo kuanzia waliposajiliwa hadi sasa. Pluijm amesema kuwa kwa upepo ambao Manji amewajaza wachezaji, mashabiki wategemee makubwa zaidi kwenye hatua ya makundi.
Pluijm ambaye ameweka rekodi ya kuifikisha Yanga hatua hiyo mara ya kwanza tangu ilipofuzu hatua kama hiyo Ligi ya Mabingwa Afrika 1998, alisema michuano hiyo inahitaji fedha nyingi ambazo Manji amekuwa akizitoa tena kwa wakati.
“Tumefuzu kutokana na mengi, wachezaji wanastahili pongezi lakini lazima tufahamu haya mashindano yanahitaji fedha nyingi, kama Manji angekuwa hatoi fedha hizo tusingefika hapa.’’ Uchunguzi wetu ulibaini Yanga kutumia kati ya Sh 70-80 milioni kwa mechi mbili dhidi ya timu moja, nyumbani na ugenini.
Gharama kubwa ni katika usafiri, kati ya Sh 35-45 milioni zimekuwa zikitumika kulingana na ukubwa wa safari kusafirisha wachezaji 23, viongozi na benchi la ufundi. Gharama nyingine ni za malazi, posho na vyakula.
MIKAKATI TU
Wakati Yanga ikitafarakari kama washiriki Kombe la Kagame litakalofanyika nchini mwezi ujao, Pluijm amesema hana papara na kwani kila kitu ni mikakati.
Alisema hatakuwa na mipango ya pamoja, ataweka mkakati wa mechi moja baada ya nyingine na kutazama ma timu yake imefanya nini.
“Sitaki kuweka presha kubwa kwa wachezaji, tunasubiri droo tuone tunapangwa na nani, mipango yetu itakuwa ni kila mechi na siyo mechi zote kwa jumla.”
WAARABU WATANO
0 comments:
Post a Comment