Mashambulizi
mawili ya mabomu katika mji wa SAMAWA ulioko kusini mwa IRAQ
yamesababisha vifo vya takriban watu 33 na kuwajeruhi wengine hamsini.
Afisa
mkuu wa polisi wa jimbo la MUTHANNA amesema mabomu mawili yaliyokuwa
yametegwa katika magari yalilipuka katika mji huo, moja likilipuka
majira ya saa sita mchana karibu na kituo cha mabasi katikati mwa mji na
la pili lilipuka dakika tano baadaye umbali wa mita 400 kutoka eneo la
shambulizi la kwanza.
Kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola
la Kiislamu IS limedai kuhusika katika mashambulizi hayo yaliyoulenga
mkutano wa kikosi maalumu cha kijeshi.
IS inayadhibiti maeneo mengi
ya KISUNNI kaskazini na magharibi mwa IRAQ na mashambulizi katika maeneo
ya WASHIA kama mji wa SAMAWA ni nadra kufanywa na wanamgambo ha
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment