Image
Image

Mkuu wa wilaya Bukombe aagiza Maafisa tarafa kusimamia hifadhi ya mavuno kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha ameagiza maafisa tarafa kusimamia kwa karibu shughuli za hifadhi ya mavuno yaliyopatikana katika Mvua za vuli Msimu wa 2015/2016 kwa kuhamasisha wananchi wenye mavuno mengi kila mahali kuhifadhi vizuri ili mavuno hayo yasiharibike na kuweka akiba ya kutosha kwaajili ya kaya zao.
Pia ameagiza Wakulima washauriwe kuuza ziada tu ya mavuno yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kila kaya isimamiwe kuhakikisha imehifadhi mazao ya chakula cha kuwatosha huku akiagiza Wafugaji washauriwe kuvuna sehemu ya mifugo yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kununua nafaka kwaajili ya kaya zao.
Amesisitiza maelezo haya yawafikie viongozi ngazi za kata,vijiji na vitongoji kwaajili ya utekelezaji na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 13/05/2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment