Rais JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anatarajia kutoa nishani maalum ya heshima kwa aliyekuwa mwanamuziki nguli wa nchi hiyo wa miondoko ya dansi nchini DR Congo,Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba (Papa Wemba) aliyefariki wiki iliyopita jijini Abidjan nchini Ivory Coast wakati akitumbuiza na anatarajiwa kuzikwa hapo kesho.
Tayari MWILI wa PAPA WEMBA ulikwisha wasili nchini KONGO ukitokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast alipofariki mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza mamia ya mashabiki na kuanguka na kukimbizwa hospitali kisha kufariki dunia.
Idadi kubwa ya watu wakiwamo mashabiki na wapenzi wa muziki walifurika katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kwaajili ya kumpokea mpendwa wao huyo nguli wa music wa dansi ambapo asilimia kubwa yawatu waliofika uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu PAPA WEMBA Wengi wao walionekana wakiwa wamevaa nguo zenye picha yake huku zikiwa zimeandikwa ‘Kwaheri Papa Wemba’.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous, alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani na mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni haswa pale aimbapo akiwa jukwaani.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) ,"Zania" (Mavuela Somo.
Mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya milele Jumanne ya wiki ijayo mara baada ya kuagwa siku ya Jumatatu.
Home
BURUDANI
Slider
Rais Kabila kutoa nishani ya heshima kwa Marehemu Papa Wemba*Kuzikwa 3 Aprili 2016 Kongo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment