Rais John Magufuli ameshusha kodi ya mapato ya mshahara (paye) kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa.
Rais
Magufuli alitangaza punguzo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akihutubia
kwenye siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa imefanyika Dodoma.
Amesema wafanyakazi wamekuwa waaminifu katika kulipa kodi ambayo inachangia kwenye maendeleo ya taifa kupitia mishahara yao.
Alisema
kwa kuwa bado vita dhidi ya wafanyakazi hewa na ufisadi inaendelea,
ataangalia namna ya kuboresha mishahara yao hapo baadaye.
“Niliwaahidi
wakati wa kampeni zangu kuwa nitapunguza kodi ya mapato kwenye
mishahara yenu;sasa natamka kuwa nashusha kodi kutoka asilimia 11 hadi
asilimia tisa.
Najua punguzo hilo litakuwa limeacha pengo kwa
serikali, lakini tutaangalia vyanzo vingine vya mapato vya kujazia
hapo,” alisema Rais Magufuli.
Kuhusu wafanyakazi hewa,Rais amesema mpaka jana idadi ya wafanyakazi hewa imefikia 10,295.
Amesema
wafanyakazi hao hewa wamelipwa zaidi ya Sh 11 bilioni na kama
wangeendelea kuachwa kwa mwaka mzima wangelipwa zaidi ya Sh 139 bilioni.
Rais Magufuli ameapa kuwashughulika popote walipo.
Pia
amewaagiza waajiri wote nchini kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao
na kuhakikisha wanapeleka michango yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
bila kukosa.
Home
News
Slider
Rais Magufuli ashusha kodi kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment