Jeshi
la polisi nchini limesema wanafunzi 78 nchini wamepoteza maisha
kutokana na ajali za barabara huku 181 wakijeruhiwa katika kipindi cha
mwaka 2015.
Hayo aliyasema leo na Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama
barabarani kutoka Makao Makuu, Fortunatus Muslim wakati wa utoaji zawadi
kwa washindi wa shindano la uchoraji alama za usalama barabarani.
Muslim
alisema kati ya wanafunzi 78 waliofariki,wavulana walikuwa 40 na
wasichana 38, huku majeruhi wakiwa 181 ambapo kati ya hao wavulana
walikuwa 81 na wa kike 81.
"Maeneo hatarishi ambayo yanaongoza kwa
kusababisha ajali za barabarani katika Jiji la Dar Es Salaam ni Lumumba,
Mnazi mmoja, Mikumi, Mtambani, Boko, Bunju na Kongowe."Alisema Muslim.
Mashindano
hayo ambayo yaliandaliwa na kampuni ya Puma Energy yalilenga kutoa
elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi juu ya utumiaji wa alama za
usalama barabarani.
"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama
barabarani limeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi, madereva na Jamii kwa
ujumla juu ya matumizi sahihi ya barabarani" aliongeza Muslim
Alisema
wanafunzi walioshinda shindano la uchoraji wa alama za usalama
barabarani ni Shaibu Abdalah kutoka shule ya msingi Gongo la mboto,
Abdallah Hussein kutoka Osterybay na Christian Mathias kutoka Gongo la
mboto.
Awali,Meneja wa kampuni ya Puma Enegy, Philippe Corsaletti
alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusiana
na matumizi sahihi ya barabarani.
Home
News
Slider
Wanafunzi 78 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabara huku 181 wakijeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment