Wakati wakazi wa Dar es Salaam wakianza kulipia huduma ya usafiri wa mabasi ya Mwendo kasi leo 16 May 2016 changamoto kadha zimejitokeza katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Abiria waliokuwa wakisubiri usafiri huo Kutoka Kimara kuelekea Kivukoni wamelalamikia utoaji huduma wa mabasi hayo nakusema hauridhishi kutokana na kuwepo ugumu wa kupata tiketi,msongamano mkubwa wa abiria vituoni hapo,utolewaji wa tiketi kama daladala pamoja na mabasi hayo ya Mwendo kasi kuchelewa kufika vituoni kwa wakati.
Wamesema kuwa kitendo cha kukata tiketi nakuanza kugombania kuingia kwenye gari za Mwendo kasi kinawakwaza kwani kunaonekana hakuna utaratibu mahususi hivyo nivyema mamlaka husika iweke utaratibu wa kueleweka kwaajili ya huduma hiyo kusudi kuepusha maswala ya uporwaji unaofanywa na vibaka wanaojifanya abiria wakati wa msongamano huo.
Wamezungumza Kauli hiyo kupitia ITV ilipofika kituoni hapo kuona halihalisi ya namna zoezi hilo lilivyoanza kazi leo ikiwa ni kwa mara yakwanza abiria hao kutozwa nauli, wengine wameenda mbali nakusema kwamba kama utaratibu niwakusuasua basi uangaliwe utaratibu wa kupangwa foleni,huku wengine wakisema tiketi hizo zinashindwa kusoma kwa wakati kwenye mashine za kukatia tiketi.
Mahojiano hapo kwa kina yatazame humu.
0 comments:
Post a Comment