Leo
3 May 2016 ni siku ya Maadhimisho ya Vyombo vya Habari Duniani yenye
lengo la kushinikiza wanahabari kuwa na uhuru usio namipaka wakati
wanaporipoti habari kwa uma badala ya kuzibwa mdomo nasehemu
nyingine,Ambapo sasa nimeipata hii kuwa Wanahabari 3 wa Kijerumani ambao
ni wapiga picha wa shirika la Ver.di wameripotiwa kukamatwa kwa madai
ya kukabiliana na polisi.
Muungano wa wanahabari nchini Ujerumani DJU umetoa maelezo na kuarifu kwamba uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na tukio hilo.
Maelezo
zaidi yanaarifu kwamba wanahabari 2 kati yao walizuiwa kwenye kituo cha
polisi kwa muda wa masaa huku mwingine mmoja akifikishwa hospitalini
kutokana na majeraha.
Polisi wanadaiwa kutumia kamba za plastiki kufunga mikono ya wanahabari hao na kutumia mabavu kuwatia mbaroni.
Kwa
upande mwingine, msemaji wa polisi wa Reutlingen alitetea maafisa wa
polisi kwa kuwashutumu wanahabari hao waliojaribu kufuata amri wakati wa
kukamatwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment