Wanawake wenye Shepu kubwa(Makalio) watetakiwa kuwaripoti vijana wanao waita "Chura" katika vituo vya polisi ili kuweza kuchukuliwa hatua baada ya kudai kuwa wanadhalilishwa jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Jeshi la Polisi wilaya ya ilala kutokana na kuibuka kwa tabia ya baadhi ya vijana kwenye mitaa mbalimbali kuwaita wanawake "Chura" huku wengine wakipiga miluzi na kushangilia.
Kuitwa kwa wanawake hao "Chura" ni baada Serikali kuufungia wimbo wa Snura Mushi uliokuwa unaitwa "Chura" kutokana na udhalilishaji wa wanawake,ambapo kwenye Video ya Wimbo huo ulikuwa ukionesha wanawake waliokuwa na Maumbo makubwa"Makalio" ambao walifananishwa na chura.
Polisi wamesema kumwiita mwanamke "Chura" ni kosa la jinai mnoo kutokana na umbo lake na kuwataka wanaodhalilishwa waripoti polisi mara moja ili tabia hiyo ikomeshwe na wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Kamanda wa Polisi wa Ilala, Lukas Mkondya akizungumza nasi kwa njia ya Simu juu ya kutaka kujua kuwa malalamiko ya wanawake hayo yamewafikia amesema kuwa kama jeshi la polisi ilala bado hawajapokea malalamiko hayo lakini ikiwa nikweli mambo hayo yapo anawataka vijana kuacha mara moja tabia ya kuwaita wanawake Chura.
Aliongeza kuwa lazima wanawake wajenge tabia ya kuheshimiana bila kujali rika, kwani kufanya hivyo ndiko kutaleta umoja, upendo na Mshikamano miongoni mwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment