Wakazi
waliojenga eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Dar es salaam leo
wamebomolewa nyumba zao ambazo ni zaidi ya nyumba 400, zoezi hilo
limekuja baada ya amri iliyotolewa na Mahakama Kuu juzi.
Taarifa
zinasema eneo hilo lenye ukubwa wa heka 33, mali ya Henry Kashangaki
lilikuwa na mgogoro tangu 1997 baada ya kundi la watu 11 kuvamia na
kuanza kujenga nyumba na kuwauzia wananchi wengine.
Baada ya eneo
hilo kuvamiwa mmiliki wake aliamua kwenda mahakamani na kuwashtaki Shaha
Matibwa na wenzake kumi, kesi hiyo iliendeshwa kwa muda wa miaka mitano
na mwaka 2010 hukumu ilitolewa na Kashangaki na Matibwa walionekana
wana haki ya kumiliki hivyo walitakiwa kugawana.
Hata hivyo,
Kashangaki hakuridhika na hukumu hiyo na kukata rufaa na kwenda Mahakama
Kuu, January 2016 kesi hiyo ilitolewa hukumu na Kashangaki alishinda,
hivyo juzi Mahakama hiyo ilitoa amri nyumba zivunjwe ili kumpisha mwenye
eneo lake.
Home
News
Slider
Zaid ya nyumba 400 zabomolewa katika eneo la Ilonganzila kwa amri ya Mahakama jijini Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment