Image
Image

Majabvi afichua mapya kwenye usajili wa Simba.

KIUNGO Mzimbabwe wa Simba, Justice Majabvi hajamalizana lolote na uongozi wa timu hiyo na amethibitisha. Majabvi alisema tatizo kubwa linalomzuia kurudi nchini ni matatizo ya kifamilia pamoja na matatizo mengine ndani ya Simba. Nyota huyo alisema kwa sasa mke wake amekwenda kusoma na mwanaye amebaki pekee hivyo anahitaji huduma yake kwa karibu jambo ambalo linamzuia kurejea nchini.

“Sijakubaliana na viongozi kama nitarudi msimu ujao maana matatizo yangu bado yapo, hizo taarifa kuwa nitarudi ni za uongo,” alisema Majabvi ambaye viongozi wa Simba wanakiri kuwa ndiye mchezaji wao bora wa msimu uliopita.

“Viongozi walikuja hapa kutafuta kocha hivyo hatukuwa na mazungumzo yoyote kuhusu mimi, siwezi kurudi kwa msimu ujao na huo ndio msimamo wangu.

“Siwezi kusema kama nitaondoka kwa mkopo ama nini lakini ukweli ni kwamba kama ningetaka kuondoka Simba ningeshaondoka kitambo, hata kukaa mpaka sasa nimejitahidi sana,” alisema Majabvi ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alishindwa kutolea ufafanuzi suala hilo kwa madai kuwa yupo likizo huku jitihada za kumpata rais wa Simba, Evans Aveva zikigonga mwamba kutokana na simu yake kutokuwapo hewani.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe aliliambia Mwanaspoti kuwa wamepanga kuendelea na Majabvi kwani alifanya vizuri msimu uliopita sambamba na kipa wao, Vincent Angban.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment