Image
Image

OPEC yashindwa kufikia makubaliano kuhusu wa uzalishaji wa mafuta ghafi

Mkutano wa 169 wa Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta OPEC umeshindwa kufikia makubaliano kuhusu kikomo cha uzalishaji wa mafuta ghafi.
Hii ni mara ya pili kwa nchi za OPEC kushindwa kufikia makubaliano kuhusu kikomo kipya cha juu cha uzalishaji wa mafuta tangu mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana.
Hivi sasa uzalishaji wa mafuta wa jumuiya hiyo uko katika kiwango cha pipa milioni 32 kwa siku.
Bei ya mafuta ya kimataifa imekuwa ikishuka, na ilishuka hadi kufikia dola 26.21 za kimarekani kwa pipa mwezi Februari, ambayo ni bei ya chini zaidi katika miaka 12 iliyopita, lakini kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Machi, bei hiyo imeanza kuongezeka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment