Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Bara la Afrika bado linakabiliwa na
changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hasa vijijini kwa
sababu nchi zake bado hazijamudu kuunganisha huduma hiyo katika maeneo
hayo.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa masuala
ya maji watafute njia sahihi itakayowezesha kutatua tatizo hilo kwa
kutumia vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoko.
Waziri Mkuu alitoa
kauli hiyo jana, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 10 wa Baraza la
Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW) ambao unaokwenda sambamba na
maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.
“Tunategemea baada ya kumazika
kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya kumaliza
tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili
kufikisha maji kwa wananchi,” alisema.
Akizungumzia kwa upande wa
Tanzania alisema, suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti
ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika
maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali
usiozidi mita 400.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki,
ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya masuala ya maji Barani
Afrika alisema maji ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi, hivyo wataalamu
wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika katika maeneo yote.
Mkutano
huo wa siku tano unahudhuriwa Mawaziri wa Maji kutoka nchi 45 za Afrika
na unaongozwa na Waziri wa Maji na Mazingira wa Senegal Amadou Mansour
Faye ambaye ni Rais wa AMCOW.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment