Waziri
Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuzindua awamu ya
kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Dodoma, ili uweze kupokea ndege
kubwa za mizigo,abiria na viongozi wa kitaifa na kimataifa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana
amesema leo waziri Mkuu atazindua ukarabati wa uwanja huo kwa Niaba ya
Rais Magufuli na kuongeza kuwa uzinduzi huo hakutaathiri ujenzi wa
uwanja wa Kimataifa eneo la Msalato.
Ujenzi na ukarabati wa uwanja
huo unatarajiwa kuhgarimu shilingi bilioni 11.5 ambazo ni fedha za ndani
na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma ikiwemo
ndege ambazo zitanunuliwa na serikali.
Rugimbana amesema kwa sababu
kubwa ya kupanuliwa kwa uwanja huo ni nia ya dhati ya rais Magufuli ya
serikali yake kuhamia Dodoma na kusema mara baada ya awamu hiyo ya
kwanza awamu ya pili itafanyika haraka ili kukamilisha mpango huo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment