Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi, Mh.Mwigulu Nchemba hii leo ameshiriki
kongamano la viongozi wa dini kuhusu matukio ya Ugaidi nchini na duniani
kote linalofanyika Serena Hotel -Dar es Salaam.
Akiongea na viongozi
hao wa dini kutoka pande zote za nchi yetu(bara na visiwani),Mwigulu
amesema "Mtu anapofanya tukio la kinyama au kigaidi akamatwe mhusika
aliyefanya hilo tukio nasio kuhusisha na dini yake,kitendo cha
kumhusisha jambazi au gaidi na imani yake ya dini kunahatarisha umoja
wetu".
Vilevile kwa upande wa serikali,Mwigulu anasema "tunaeendelea
kuchukua hatua za kupambana na matukio ya kinyama na yanayoashilia
ugaidi,tunaomba viongozi wote wa dini kwa ngazi zote tuendelee kufanya
kazi kwa pamoja kuanzia ngazi ya juu hadi chini kabisa ilikuimarisha
usimamizi wa usalama wa raia,makazi na nyumba zetu za ibada".
Viongozi
wanaoshiriki kongamano hilo ni pamoja na Mufti mkuu wa Tanzania ,Shekhe
mkuu wa mkoa wa Dsm, Askofu mkuu wa KKKT Alex Malasusa,Mashekhe na
maaskofu mbalimbali.
Home
News
Slider
Serikali imesema ipo imara kupambana na wafanyaji matukio ya kinyama na kuogofya jamii.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment