Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman amesema anatambua uchakavu
wa mahakama hapa nchini pamoja na mlundikano wa kesi uliopo na
atahakikisha kero hizo sugu za mahakama zinaisha haraka iwezekanavyo.
Amesema
lengo la Mahakama ni kuhakikisha kuwa haki inatendekea kwa haraka na
kwawakati huku wafanyakazi wa idara hiyo wakifanya kazi katika mazingira
yaliyo bora na rafiki kwao.
Jaji Mohamed Chande amebainisha yayo
wakati alipo maliza kutembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Kailima Ramadhan Kombwey
amewaambia waandishi wa habari katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere
na kuongeza kuwa katika banda la tume hiyo kuwa wataendelea kusimamia
vyema chaguzi mbalimbali nchini bila kupendelea chama chochote.
Home
News
Slider
Chande Othman:Natambua mlundikano wa kesi uliopo na uchakavu wa Majengo nitashughulikia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment