SIKU
moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Bavicha), kutangaza kuzui mkutano mkuu maalumu wa CCM utakaofanyika
Julai 23, mwaka huu, vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) nao wamejibu
mapigo.
Umoja huo wa vijana wa CCM umesema, ikiwa Bavicha watathubutu
kufanya vurugu hizo wanaweza kujuta na UVCCM haitasita kupita juu ya
nyayo zao ili kukihami chama chao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo, Shaka Hamdu Shaka, alisema kama
Bavicha wataamua kuendeleza siasa za kishetani zinazohusisha hujuma,
kutishia maisha, kujenga hofu kwenye jamii au kuiingiza nchi katika
vurugu, watawakabili kwa nguvu zao.
Alisema ikiwa baraza hilo
limeelekezwa na viongozi wao kufanya siasa za vurugu, mapigano au ghasia
kama njia ya kujijenga kisiasa, UVCCM itajibu mapigo kwa gharama ile
ile watakayoitumia.
“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na
wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami chama, kulinda viongozi wake
na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Shaka.
Alisema mataifa
yote yaliyoendelalea kiuchumi na kidemokrasia yamefikia malengo yake
baada ya kutenganisha vipindi vya siasa na vya kujijenga kiuchumi hivyo,
Tanzania nayo haitakubali kuendeleza malumbano ya kisiasa na kupoteza
muda kwenye mambo ambayo msimu wake umepita na kuacha kusaka maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment