KANISA
la Good News for All Ministry limeanza utaratibu wa kufanya maombi kila
siku ya Jumanne kwa siku 1,001, ikiwa ni mwitikio wa kumuombea Rais
John Magufuli afya njema na ulinzi wa Mungu ili aweze kutimiza majukumu
yake mazito ya kulitumikia taifa.
Akiongoza maombi katika viwanja vya
Biafra jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Good News for All Ministry,
Askofu Dk Charles Gadi alisema wameamua kuchukua jukumu hilo kuitikia
ombi la Rais Magufuli akitusihi Watanznaia tumuombee.
Rais alisema
maombi ya Watanzania yanamtia nguvu katika kazi yake ya kuhakikisha nchi
inaendeshwa kwa kuzingatia misingi imara ya kiutawala.
“Tunamuombea
Rais ili aweze kufanikiwa katika juhudi zake za kurekebisha uchumi wa
nchi, pia tunaombea lengo la Rais wetu la kuifanya nchi yetu iwe ya
viwanda vikubwa na vidogo ili kila mahali katika nchi yetu, wananchi
wapate kazi na pia tuweze kuuza nje bidhaa za viwandani na kupunguza
utegemezi wa kuagiza bidhaa hizo nje,” alisema.
Aidha, alisema
wanawaombea wasaidizi wakuu na viongozi wengine wa nchi ili waweze
kumsaidia katika kasi aliyonayo ya kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano
sambamba na kumuomba Mungu alete mvua isiyo ya uharibifu wa mali na watu
nchini.
“Katika maombi haya pia tunawasihi na kuwahamasisha wananchi
kuwa na utayari wa kulipa kodi na ushuru ili kukuza uchumi na maendeleo
ya nchi, jambo ambalo pia ni uzalendo kwa nchi yetu”. “...Tunaombea na
kuhamasisha wananchi wetu wawe walinzi wa miundombinu ili iweze kudumu
na kuhudumia vizazi vijavyo,” alisema.
Hata hivyo alisema katika
maombi hayo pia watahamasisha wananchi kulinda maadili ya kitaifa na
kijamii na kujiepusha na tabia zinazoleta mmomonyoko wa maadili kwa watu
wazima na watoto.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment