Uturuki yatangaza hali ya hatari.
Ni siku ya pili leo nchini Uturuki baada ya kutangazwa sheria ya hali ya hatari. Msemaji wa serikali Numan Kurtulmus amesema sheria ya miezi mitatu ya hali ya hatari iliwekwa kwa lengo la kufuatilia mfumo sambamba wa uongozi unaotumiwa na kiongozi wa kidini Fethullah Gulen, anayeshutumiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.
Gulen amekana kuhusika na jaribio la mapinduzi la siku ya Ijumaa iliyopita, ambalo limesababisha zaidi ya watu 260 kuuwawa na wengine 1,500 walijeruhiwa.
Naibu waziri mkuu wa Uturuki Mehmet Simsek amesisitiza kwamba sheria ya hali ya hatari haitazuiwa misingi ya uhuru, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kutembea, kukusanyika kwa watu na uhuru wa vyombo vya habari. Bunge lilitarajiwa kukutana leo kujadili kuhusu sheria hiyo ya hali ya hatari.
0 comments:
Post a Comment