KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa neno
endapo Rais John Magufuli atamhitaji kuendelea na wadhifa huo, huku
akibainisha kuwa amekutana na changamoto nyingi katika nafasi hiyo kiasi
kwamba wakati mwingine alikata tamaa.
Mwanasiasa huyo maarufu ndani
ya CCM na nchini, anatarajiwa kuhitimisha uongozi wake wiki hii wakati
Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, Rais John Magufuli atakapokabidhiwa
uenyekiti huo na kuunda Sekretarieti yake mpya ambayo haijulikani kama
itaongozwa tena na Kanali huyo wa zamani wa Jeshi.
Akizungumza jana
na waandishi wa habari baada ya kukagua Ukumbi wa Mkutano Maalumu wa CCM
utakaofanyika keshokutwa Jumamosi, Kinana ambaye amekuwa katika nafasi
hiyo kwa miaka mitatu na nusu, alisema aliombwa katika nafasi hiyo baada
ya kuwa aliamua kustaafu, lakini akakumbana na changamoto mbalimbali.
CCM
kuwa mbali na wananchi Alisema kuna wakati aliona kama vile chama
kiliacha kwenda kwa wananchi na kwamba hakikuwa karibu sana nao.
“Ninyi
ni mashahidi, ikabidi kubuni utaratibu mzuri wa kwenda kwa wananchi ili
chama kiwe karibu na wananchi, kiwasikilize na kuwa sauti ya wananchi
kifuatilie matatizo yao kisimamie utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,”
alisema Kinana na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo amekuwa
akiwasiliana na Rais na Waziri Mkuu kwa ajili ya matatizo kutatuliwa.
“Changamoto
ya pili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, hapo nyuma
kulikuwa na misukosuko kidogo ya umoja na mshikamano, kushutumiana na
kulaumiana,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine aliyofanya ni
kuimarisha umoja ndani ya chama, kushirikiana na viongozi wenzake
kuhakikisha chama kinajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kurejea katika
misingi yake ya awali katika maeneo ya uadilifu, uwajibikaji na utendaji
kazi kwa ufanisi.
Azuiwa ziarani
Kinana alisema amekwenda wilaya
zote, majimbo, mikoa na nusu ya kata za nchi na amesafiri zaidi ya
kilometa 192,000, kufanya mikutano zaidi ya 3,700 ya aina mbalimbali ya
ndani na nje na haikuwa kazi rahisi “Changamoto nilizokutana nazo ambazo
lazima nikiri ni pale nilipotaka wakati mwingine kufanya ziara kwenye
maeneo fulani fulani niliambiwa ni hatarishi siwezi kwenda kwa hiyo
ilibidi nibishane na viongozi na watendaji wakuu wa serikali…nikasema
hapana nimeamua kwenda lazima niende,” alisema Kinana.
Katibu huyo
akitoa mfano alisema kuna wakati aliamua kutoka kwa boti kutoka
Nyamisati wilayani Rufiji kwenda Mafia, viongozi wa Mkoa wa Pwani
walifikiri si njia salama ya kusafiri na kumpelekea ujumbe asisafiri kwa
boti, bali asafiri kwa ndege, lakini alisema hapana ataondoka kwa boti.
“Walichofanya
wakakaa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wakaniandikia
barua rasmi kwamba tunakushauri usisafiri kwa boti safiri kwa ndege kwa
maana nyingine walikuwa wanajivua lawama kwa yatakayotokea, lakini vile
vile kunitisha kidogo kwamba si salama zaidi nikawasisitiza hapana,”
alieleza Kinana.
Ashitakiwa kwa JK
“Baadaye Rais mstaafu Kikwete
alikuwa Msoga, viongozi wa Mkoa wa Pwani wakaenda kumwambia tumezungumza
na Katibu Mkuu wako naona hasikii tumemuandikia barua ya kumuomba
asisafiri na boti hasikii, Rais akaandika meseji ndefu sana…nikamjibu
rais nakuheshimu mamlaka yako ni makubwa si vizuri nikakukatalia, lakini
niruhusu nikukatalie kwa sababu hata wananchi wanaosafiri kwenye boti
hii wanahatarisha maisha yao, ni vizuri na mimi nikahatarisha maisha
yangu hata kidogo… akaniambia nimekuelewa endelea,” alibainisha.
Alisema
zipo changamoto nyingi sana nyingine, kwa mfano Mbambabay kwenda Kyela,
mkuu wa mkoa akamuambia boti haifai kusafiri akasema mara haiwezi
kusafiri imeharibika.
“Nikazungumza na Mwakyembe akapeleka mafundi
wakatengeneza, safari haikuwa rahisi, lakini changamoto zilikuwa nyingi
sana, kwingine Lupingu kule ni gari moja tu ndio inayoshuka chini hakuna
kupishana magari nikaambiwa nisiende nikasema nina kwenda,” alisema na
kuongeza kuwa kulikuwa na ubishi mwingi wakati mwingine alionekana mtu
mmoja kidogo ambaye hasikilizi ushauri sana.
Pia nyingine
zinazotokana na changamoto za wananchi kutolipwa mazao yao kwa wakati,
mbolea kutofika kwa wakati, halmashauri kutopata fedha za maendeleo kwa
wakati, watumishi wa umma wanaohamishwa kwenda vijijini hawaendi
vijijini kwenda kuwahudumia wananchi, tatizo kubwa la migogoro kati ya
wakulima na wafugaji kati ya wananchi na hifadhi za taifa.
“Ndio
maana mnaniona siku hizi nimenyamaza kwa sababu yale yote niliyokuwa
nikiyaombea yanafanyika, umangimeza haupo watu wachape kazi wawahudumie
wananchi, uadilifu unapigwa vita, rushwa inapigwa vita, uwajibikaji na
uadilifu unahimizwa, utendaji kazi unatakiwa na hayo yasipofanyika mtu
anaondolewa mara moja,” alifafanua Kinana ambaye kuanzia mwaka 2014 hadi
mwanzoni mwa mwaka jana alitembea kote nchini akikisafisha chama chake
na kuibana serikali.
Kurejea kwake CCM
“Yalitokea mazingira ambayo
niliombwa na viongozi wastaafu na viongozi wa chama kuniomba niwe
mtendaji mkuu wa chama chetu. Si nafasi ambayo niliipenda, bali niliitwa
na nikakalishwa wakanisihi na mimi nikakubali sababu ni wito na kwa
kuwa ni watu ninaowaheshimu na wana dhamana kubwa kwenye nchi yetu,
nikakubali kufanya kazi hiyo,” alisema Kinana akizungumzia jinsi
alivyoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Alisema amekuwepo katika uongozi
ndani ya chama kwa muda mrefu (miaka 25) ndani ya Kamati Kuu na
Halmashauri Kuu ya Taifa, na alihisi ni wakati muafaka wa kung’atuka.
“Mwanasiasa
mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Ni wakati
mzuri wa kung’atuka kuachia waingie wenye umri wa kati na umri wa
vijana kuachia waongoze chama na kuwaamini,” alieleza.
Alisema moja
ya mambo ambayo walikubaliana wakati ule akajitahidi kukiimarisha chama,
kusimamia na kumsaidia mwenyekiti kusimamia mchakato wa kuwapata
wagombea kwenye nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Pia alijitahidi
kuendesha shughuli za kampeni na uchaguzi na utakamalizika.
“Uchaguzi
umekwisha niruhusiwe kupumzika, na wote waliafiki na kukubali sasa muda
umefika kwa hiyo nimewakumbusha yale tuliyokubaliana muda wake umefika
sasa wengine wakaniuliza hivi ndivyo tulivyokubaliana nikawaambia wazee
hamjawa wazee kiasi cha kusahau ndio haya tuliyokubaliana,” alieleza.
Akiombwa na JPM
Alipoulizwa
kama akiombwa na Rais Magufuli aendelee kwa Katibu Mkuu, Kinana
alisema, “Niseme hajasema, hatujazungumza hilo, likitokea tutaangalia,
tutakaa naye kikao kama akiniomba, tutakuwa na kikao na mazungumzo muda
utakapofika kama nilivyokuwa na mazungumzo na kikao kama kwa wale
walioniomba mwaka 2012.”
Waliokisaliti chama
Akizungumzia
walioisaliti CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mtendaji huyo wa CCM
alisema msaliti yeyote adhabu yake ni mbaya sana, hata kwenye chama cha
siasa.
“Kwenye CCM wapo watu walioyumba, kulikuwa na wimbi kubwa
mwaka jana, watu waliyumba hivi kidogo wakakaa mguu upande huku hawapo
na kule hawapo, wako ambao sio tu waliyumba, bali walikiuka maadili na
hawakushiriki kwenye shughuli za kampeni,” alisema.
Pia alisema wapo
ambao hawakushiriki, hawakusaidia na wakasaidia upinzani na kila mtu
atakuwa na adhabu yake kulingana na makosa yake.
“Kama mmekuwa
mkifuatilia kuna waliochukuliwa hatua ngazi za wilaya na mikoa. Kwa
mfano, Shinyanga 123 walichukuliwa hatua. Wapo wanaotakiwa kuchukuliwa
hatua kwenye ngazi za juu, sasa jambo moja mtu yeyote kabla ya
kuchukuliwa hatua lazima aelezwe mashtaka yake, apewe fursa ya
kusikilizwa, kwa hiyo hawa wote watasomewa mashtaka, watasikiliza na
kupewa adhabu kwa kadri itakavyostahili, lakini hatua zitachukuliwa mara
baada ya Mkutano Mkuu kumalizika,” alieleza.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment