Siku
tatu za mkutano mkuu wa chama cha upinzani nchini Marekani cha
Republican zitafikia kilele hii leo, wakati mgombea rasmi wa chama
hicho Doland Trump atakapotoa hotuba muhimu akikamilisha miezi 13 ya
kampeni kutaka kuteuliwa na chama hicho kugombea urais nchini
Marekani.
Trump atapata fursa ya mwisho leo kujaribu kutoa
taswira ya urais kabla ya mtazamo kuhamia katika mkutano mkuu wa
chama cha Democratic wiki ijayo.
Jana gavana wa jimbo la Indiana Mike Pence alikubali uteuzi wake kuwa mgombea mwenza wa Trump.
Seneta
wa Texas Ted Cruz aliyewania nafasi hiyo pamoja na Trump katika
kura za mchujo jana alikataa kumuidhinisha mgombea huyo wa chama
cha Republican katika hotuba yake kwa wajumbe, na kuzusha hali
ya kuzomewa na waungaji mkono wa Trump na kuvuruga hali ya
umoja wa chama hicho ambayo ilianza kujengeka mjini Cleveland
wiki hii.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment