Leo
Julai 21 ni mwaka mmoja tangu Pierre Nkurunziza alipochaguliwa tena
kuiongoza Burundi kwa kipindi cha miaka 5, licha ya upinzani kukosowa na
kudai ya kuwa katiba ya Burundi haikumruhusu kuwania muhula wa tatu.
Utata
huo ulisababisha maandamano ya kupinga azma yake, na mauwaji ambayo
Umoja wa Mataifa unakadiria yameuwa watu zaidi ya 500. Licha ya usalama
kuonekana kurejea hatua kwa hatua kiuchumi nchi inaelezewa kuwa katika
hali ngumu kufuatia hatua ya wafadhili wakuu kusitisha misaada ya
kifedha. Changamoto kubwa zaidi hata hivyo ni kutopigwa hatua yoyote
katika majadiliano ya kisiasa yenye lengo la kumaliza mzozo unaoikabili
nchi hiyo kwa mwaka mmoja sasa.
Mwaka mmoja tangu kufanyika uchaguzi
Rais Pierre Nkurunziza na serikali yake wameonekana kuimarika kitaifa.
Waziri wa usalama Alain Guillaume Bunyoni amesema wamefaanikiwa kupiga
hatua kubwa kwa kukabiliana na walokuwa wakiyumbisha usalama.
"Makundi
yaliyokuwa yakiendesha uhalifu, silaha zilikuwa zinamilikiwa kinyume na
sheria zimeshikwa na mamlaka ya polisi. Na bunduki za aina nyingi zaidi
ya 164,guruneti 199, na mabomu kadhaa vimekamatwa, magaidi 35
walijisalimisha mamlaka za usalama" amesema waziri Bunyoni.
Hali ikoje sasa?
Licha
ya hatua hiyo, mauwaji yakuvizia bado yame shuhudiwa, tarehe 13 mwezi
huu aliuwawa mchana kweupe Mbunge Hafsa Mossi zamani muandishi wa
habari, mwenye umaarufu kitaifa ,kikanda na kimataifa. Hadi sasa sababu
za kuuwawa kwake bado zimesalia gizani.
Halmashauri ya Umoja wa
mataifa inayo husika na haki za binaadamu imekadiria kuuwawa kwa watu
zaidi ya 500 katika kipindi cha mwaka huu mmoja.
Wakati serikali
ikionekana kuweka nguvu katika kurejesha usalama, raia walalamika kuumia
kiuchumi ambapo faranga ya Burundi yashuhudiwa kuporomoka thamani
ukilinganisha na pesa ya kigeni. Baadhi ya wananchi wa mjini Bujumbura
wanasema kuwa maisha yamezidi kuwa magumu hasa katika masoko kwa kuwa
bidhaa zinapanda bei. Hii ni baada ya wahisani wakuu kusimamisha misaada
ya kifedha.kamwe serikali haitoketi kwenye meza moja ya majadiliano na
walohusika na jaribio la kutaka kuipindua serikali kwa sababu kwa
kufanya hivyo itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali.
Mazungumzo ya amani
Baada
ya vikao kadha kufanyika Arusha tangu kuteuliwa Benjamin Mkapa rais
Mustaafu wa Tanzania kuwa mpatanishi bado serikali ya Burundi kupitia
waziri wa mambo ya nje Alain-Aime Nyamitwe amekumbusha kuwa kamwe
serikali haitoketi kwenye meza moja ya majadiliano na walohusika na
jaribio la kutaka kuipindua serikali kwa sababu kwa kufanya hivyo
itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali. Wahisani wameweka kigezo kikuu
ni kupiga hatua kwenye majadiliano jumuishi yenye dhamira ya kumaliza
mzozo huo ulozuka leo mwaka mmoja. Matarajio ya raia wa Burundi ni kuona
mgogoro huo unatafutiwa jawabu kwa wanasiasa wote kuketi chini na
kumaliza tofauti zao ili amani iweze kurejea.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment