Ujerumani
na Uingereza zimekubaliana kwamba waziri mkuu mpya Theresa May
anahitaji muda wa kutayarisha mazungumzo ya kujitoa kutoka Umoja
wa Ulaya, baada ya nchi hiyo kuchukua hatua ya kwanza kuelekea
kile kinachojulikana kama Brexit kwa kuachia urais wa Umoja wa
Ulaya.
Katika ziara yake ya kwanza ya kiserikali nje ya
nchi, May alikutana jana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
mjini Berlin.
May alisema Uingereza itasubiri hadi takriban
mwishoni mwa mwaka huu kuchukua hatua za mwanzo za kujitoa
kutoka Umoja huo, na kuanzisha kifungu cha 50 cha mkataba wa
Lisbon. May alizungumzia pia kuendeleza uhusiano mzuri na Ujerumani
pamoja na mataifa yote ya Umoja wa Ulaya.
Waziri mkuu huyo wa
Uingereza anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya nje nchini
Ufaransa leo ambako anatarajiwa kukutana na Rais Francois
Hollande.
Home
Kimataifa
Slider
May anahitaji muda wa kutayarisha mazungumzo ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment