Serikali
ya Tanzania imesema imewapeleka madaktari wa magonjwa mbalimbali nchini
India kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu ili kupunguza wimbi la
wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje kwa gharama za serikali.
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Wizara ya ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema hatua pia
itasaidia kusaidia sekta ya Afya kwa kiasi kikubwa.
Aidha Dkt.
Ulisubisya amesema tayari serikali imeziagiza taasisi mbalimbali za
kiserikali zinatoa huduma za kiafya kuboresha mazingira ya watumishi wao
ikiwemo kutoa motisha kwa wafanyakazi hao kupitia mapato ya ndani ya
taasisi zao ili koboresha zaidi huduma za kiafya kupita watumishi hao.
Amesema
kuwa upungufu wa madaktari hao ambao wameenda kupata uzoefu ni pamoja
madaktari katika idara ya Koo,Pua, Masikio, Figo, na Tumbo ambapo
watakaporejewa kutakua hakuna ulzima wa kuwasafirisha wagonjwa wenye
matatizo hayo kwenda nje ya nchi.
Katibu Mkuu amesema pia Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ipo katika mpango wa kuboresha mejngo yake ikiwa
ni pamoja na kuongeza vyumba vya uapsuaji kwa watoto ili kuondoa
mlolongo mrefu wa watoto hao kufanyiwa upasuaji.
Ameongeza kuwa pia
huduma ya magonjwa ya nje kwa tafiti walizofanya imeboreka kwa kuwa
madaktari kwa wanapatikana muda wote kutoa huduma kwa wagonjwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment