Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kuundwa kamati za amani nchini zitakazo saidia kuondoa tofauti na kuleta maelewano baina ya waisilamu na wakristo. “Dini
ndiyo inayojenga msingi imara kiroho, kiimani na ndiyo inajenga maadili
mema. Leo tunaposema kila mtu awe muadilifu tumegundua ili tufanikiwe
lazima tuweke mazingira mazuri yatakayowezesha madhehebu yote kuabudu
kwa uhuru,” alisema.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo , wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na
wananchi wa vijiji vya Malolo na Chimbila ‘B’ akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya kukagua shughuli za maendeleo
wilayani Ruangwa.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imegundua
kuwa ili iweze kufanikiwa ni lazima ishirikian na madhehebu ya yote ili
yaweze kufanya kazi zake vizuri.
“Nikiwa mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali niliamua kuunda kamati ya amani ya Taifa ambayo inajumuisha
viongozi wa dini zote. Pia nimeiagiza mikoa na wilaya zote kuunda
kamati za amani ili kuhakikisha umoja na maelewano miongoni mwa dini
zote nchini unakuwepo,” alisema.
Alisema
lengo la kamati hizo za amani ni kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa
na maadili mema na kutambua umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu
nchini.
Akizungumzia
tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji
vya Nanganga, Nangumbu, Mbecha, Malolo, Mpumbe na Chimbila ‘B’ alisema
Serikali inalifanyia kazi suala hilo.
Alisema tayari mtaalamu wa kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi ameshawasili katika wilaya hiyo na baada ya kukamilisha utafiti huo shughuli ya uchimbaji visima itaanza.
Waziri
Mkuu alisema lengo la utafiti huo ni kutaka kubaini wingi na ubora wa
maji katika eneo husika hivyo aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa na
subira wakati suala hilo likishughulikiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment