>>>BAADHI ya mitambo, nguo na malighafi za kutengeneza nguo katika kiwanda cha nguo cha 21st Century kilichopo Kihonda, Manispaa ya Morogoro, zimeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa ambayo bado haijafahamika.
Akizungumzia
moto huo, Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Clement Munisi, alisema
ulizuka juzi saa 12:00 asubuhi katika mashine moja ya kutengenezea nguo.
Alisema moto huo ulianza kwa kutoa cheche na wafanyakazi walijaribu kuuzima kwa kutumia kifaa maalumu cha kuzima moto (Fire extinguisher ) bila ya mafanikio.
Alisema moto huo uliunguza baadhi ya mitambo na malighafi zilizokuwa katika chumba kimoja katika kiwanda hicho na kusababisha hasara kubwa.
Munisi alisema moto huo uliendelea kuenea katika vyumba vingine na kusababisha baadhi ya nguo zilizokuwa zikiendelea kutengenezwa katika mitambo kuungua na kusababisha hasara ambayo hadi hivi sasa thamani yake bado haijafahamika.
Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Ramadhani Pilipili, alisema licha ya kikosi hicho kuwahi kufika katika eneo la tukio, miundombinu ya kiwanda hicho ni kikwazo katika kuukabili.
‘’Miundombinu ya kiwanda ni tatizo kutokana na kukosekana na eneo sahihi la kupitishi mipira ya maji na hivyo kulazimika kutumia muda mwingi kuvunja ukuta ili kufanikisha uzimaji,” alisema.
Alisema changamoto hiyo imepelekea uzimaji kuwa gumu, kwani eneo la moto ulikoanzia kuwaka halijafikiwa isipokuwa eneo la pembezoni.
Alitoa wito kwa uongozi wa kiwanda kuweka miundombinu ya mabomba juu ya paa ili ikitokea tena tatizo kama hilo iwe rahisi kutatua.
Naye mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini, alisema huu ni mwezi wa tatu tangu mojawapo ya mashine inayotumika kuzalishia nguo kuwa na tatizo la kutoa cheche na hivyo wafanyakazi kulazimika kuzima mara kwa mara inapoonekana inatoa cheche za moto kutaka kuleta madhara.
Ofisa Mazingira wa kiwanda hicho, Anna Gervas, alisema wafanyakazi wa kiwanda hicho wako hatarini kukosa ajira kutokana na uharibifu uliosababishwa na moto huo jambo linaloweza kupelekea kiwanda hicho kufungwa kwa muda.

0 comments:
Post a Comment