Image
Image

Mtoto mwenye betri moyoni atolewa ICU.

AFYA ya mtoto Happiness Josephat (5), aliyewekewa betri ya kuendesha moyo mwishoni mwa wiki katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeendelea kuimarika baada ya kuondolewa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kulazwa katika wodi za kawaida.

Upasuaji huo unaojulikana kwa jina la ‘Pecemaker Insertation,’ ulifanyika kwa mara ya kwanza nchini na kufanikiwa kumuwekea betri baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi.
“Afya ya mtoto imeimarika zaidi na inaimarika kila siku, leo anaondolewa ICU na kwenda kulazwa katika wodi ya kawaida,” Ofisa Habari wa taasisi hiyo, Maulid Mohamed, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Mohamed alisema upasuaji huo umeonyesha mafanikio makubwa baada ya Happines kuonyesha dalili za kuendelea vizuri baada ya upasuaji.
Taasisi hiyo iliyozinduliwa Septemba mwaka jana na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, pia inatoa mafunzo ya ubingwa wa juu katika fani ya upasuaji wa moyo, usingizi na tiba ya moyo.
Januari hadi Agosti, mwaka huo, ilihudumia wagonjwa wa nje 14, 257, wagonjwa waliolazwa ni 912 na ilifanya upasuaji kwa wagonjwa 148.
Kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watano (sawa na asilimia 3.4), walifariki dunia, kiwango ambacho ni kidogo kuliko wastani uliokisiwa na wataalam wa asilimia 13.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment