Wakiwa
katika uzinduzi wa sekta ya usafirishaji iliyowahusisha waendesha
bodaboda wa Wilaya za Siha na Manispaa ya Moshi, wanawake hao walisema
licha ya kuamua kujikita rasmi katika ajira hiyo ili kujipatia kipato,
nia yao kubwa ni kuidhihirishia jamii utegemezi ni tabia ya kutopenda
kujishughulisha.
Walitoa msimamo huo jana, baada ya kumalizika kwa mafunzo ya wiki nane yaliyoandaliwa na Shirika la Kijamii la Tusonge kuhusu masuala ya udereva kwa vitendo, alama za barabarani, sheria za barabarani na njia nyingine za usafirishaji.
Mmoja wa madereva hao, Janeth Baitan, alisema anajua kazi hiyo ni hatari, lakini kwa sababu anatamani jamii ibadilike kimtazamo, iachane na hisia mbaya dhidi ya wanawake, anataka kutumia uthubutu huo ili aweze kukabiliana na changamoto ya ajira, hali ngumu ya maisha, mfumo dume na udhalilishaji.
“Kuendesha kwangu bodaboda ndio chanzo cha mapato yangu ya kila siku yanayoniwezesha kuendesha maisha katikati ya kundi kubwa la vijana wenye tatizo la ajira linalozidi kukua kila siku. Hiki ndicho kipato changu halali na nitapambana na mfumo dume hadi tutakapofanikiwa kiuchumi,” alisema Upendo Njau.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kijamii la Tusonge, linalojihusisha na uwezeshaji kiuchumi wanawake na makundi ya vijana katika maeneo ya pembezoni, Agnatha Rutazaa, akizindua mafunzo hayo, alisema katika kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, wameanzisha kampeni ya kutoe elimu kwa waendesha bodaboda ambao ndio waathirika wakubwa.
Alisema vijana wengi wamejiingiza kwenye biashara hiyo, huku baadhi yao wakitumia vyombo hivyo vya moto bila tahadhari kutokana na kutokuwa na elimu ya usalama wa barabarani hali inayosababisha baadhi yao kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hadi sasa jumla ya waendesha bodaboda 40 wameshapigwa msasa.
“Tulipanga kuwapa elimu ya usalama barabarani vijana 30, lakini kutokana na wengi kuhitaji elimu hiyo tulifanikiwa kuwapata vijana 40 ambao kati yao wasichana ni wanane na wavulana ni 32.
Wanawake hawa wamezua gumzo hasa kutokana na udogo wa maumbile yao na hata uthubutu wao wa kushindana na wanaume kunyang’ang’anyana abiria vijiweni,” alisema.
Madereva hao wa bodaboda kutoka Wilaya ya Siha na Kata za Msaranga na Majengo za Manispaa ya Moshi, walianza kupigwa msasa na askari wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro, kati ya mwezi Aprili na Juni, mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment