Mtu
mmoja aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye
Treni Kusini mwa Ujerumani usiku wa jumatatu na kuwajeruhi watu wanne
kabla yeye kupigwa risasi na Polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya
tukio hilo.
Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao
wa Facebook kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14
wanapata msaada wa kitabibu kutokana mshtuko walioupata.
Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.
vyombo
vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani
mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye
asili ya Afghanistan.
Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji
milioni moja waliokuwa wakiingia nchini humo, zaidi ya 150,000 raia wa
Afghanistan.
Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa
kiislamu nchini Ufaransa, kumekuwa na hali ya hofu ya kutokea
mashambulizi kama hayo nchini Ujerumani, lakini mpaka sasa hakuna ishara
zozote kuwa shambulio hilo lilikua la kigaidi.
Home
Kimataifa
Slider
Mtu mmoja aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni Ujerumani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment