Shule 70 za upili zimeteketezwa moto na wanafunzi wenye hasira nchini Kenya.
Waziri
wa elimu nchini humo Fred Matiangi ameiambia kamati ya bunge iliyoundwa
kupeleleza wimbi la shule kuteketezwa kuwa hakujakuwa na hata wanafunzi
20 waliohukumiwa kwa kuteketeza mali ya umma kwa sababi moja au
nyingine kati ya visa 317 zilizoripotiwa kati ya mwaka wa 2007 -2016.
''Endapo
serikali itachukua hatua dhidi ya wale watakaoteketeza mabweni yao au
hata madarasa bila shaka wale wanaoiga wataogopa'' alisema bwana
Matiangi.
''Mara nyingi tumegundua kuwa zile shule ambazo
zinachunguzwa kwa sababu ya wizi wa pesa za kufadhili masomo ya bure na
fedha za kununua vitabu vya wanafunzi zinateketezwa kwa sababu finyu
sana''.
Walimu 15 wakuu wanachunguzwa kulingana na taasisi inayosimamia walimu nchini Kenya TSC.
Wandani
wa maswala ya elimu nchini Kenya akiwemo katibu mkuu wa muungano wa
walimu KNUT bwana Wilson Sosion amelaumu mabadiliko ya sera yaliyotolewa
na wizara ya elimu kama vile kuongeza muda wa muhula wa pili, na kupiga
marufuku likizo ya kati ya muhula ujao mbali na kupiga marufuku wazazi
kuwatembelea wanafunzi shuleni kama sababu zinazochochea wimbi hili la
moto shuleni.
Hata hivyo waziri Matiang'i akijitetea aliiambia kamati
hiyo ya bunge kuwa kabla ya mabadiliko hayo kutangazwa shule 90
zilikuwa zimeteketezwa tayari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment