May
28 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa
wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu
Dodoma.
Wanafunzi waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika
katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 6,595
waliodahiliwa katika Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari
na kundi la pili lilikuwa na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika
mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi.
Taarifa
iliyotolewa leo na waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Joyce Ndalichako amesema kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa
wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanya Uchambuzi wa wanafunzi
hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Baada ya uchambuzi huo leo
July 19 2016 Serikali imetangaza maamuzi haya…….
Kundi la Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari
Serikali
imesema kwa kuwa uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa
Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa
kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II – 248), wanafunzi
hao ndiyo pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili
wakamalizie mafunzo yao katika Chuo hicho.
Wanafunzi 4,586 wa mwaka
wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari
waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya Ualimu vya
Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.
Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.
Wanafunzi
290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma Programu Maalum ya Stashahada ya
Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana
sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo
nazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao.
Kundi la Programu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi
Serikali
imesema wanafunzi katika kundi hili hawakuwa sehemu ya program maalum
ya kupunguza uhaba wa walimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati.
Walikuwa wanaandaliwa kufundisha shule za msingi wakati lengo la
Programu Maalum ilikuwa ni kukabiliana na tatizo za uhaba wa walimu wa
Sekondari. Maudhui ya program waliyokuwa wanasoma hayakuwa sawasawa na
yale ya Programu ya Ualimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi
29 wa mwaka wa II wenye Cheti cha Daraja IIIA waliodahiliwa kusoma
Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi watahamishiwa katika Chuo cha
Ualimu Kasulu wamalizie masomo yao kwa gharama zao wenyewe.
Wanafunzi
1,181 waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Kawaida ya Ualimu wa Elimu ya
Msingi waombe mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo mahali popote
watakapotaka wao.
Aidha Serikali imesema itaendelea kuwapatia mikopo
wanafunzi watakaorejeshwa UDOM na wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo
vya Ualimu vya Serikali watapewa mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa
mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya Ualimu itakayolipwa moja kwa moja
Chuoni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment