Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii
huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua sekta ya sanaa yeye
binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye kukiuka
maadili.
“Kazi
zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na
kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.”
Ameeleza
ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA
namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda
maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi
yoyote ya sanaa.
“Ikumbukwe
kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana
na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi
kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya
matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa
maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye
kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa
Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Katipatamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.”
0 comments:
Post a Comment