Theresa May hii leo atakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke katika historia ya Uingereza, wakati David Cameron akiondoka madarakani baada ya wapiga kura wa Uingereza kuamua kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Waziri
Mkuu David Cameron atahudhuria kikao cha mwisho cha kujibu masuali
bungeni kabla ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia
Elizabeth wa pili katika Kasri la Buckingham.
Malkia kisha atamtaka
May, ambaye kwa sasa ni waziri wa mambo ya ndani, kuunda serikali na
waziri huyo mkuu mteule atatoa taarifa nje ya makaazi yake mapya ya
Downing Street. Viongozi wa Ulaya wameitaka serikali ya Uingereza kuharakisha mchakato wa kujitoa rasmi katika umoja huo, lakini May amedokeza kuwa hatauharakisha mpango huo, mashuhuri kwa jina la Brexit.
May,
aliye na umri wa miaka 59, atakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke wa
Uingereza baada ya Margaret Thatcher ambaye kila mara hulinganishwa
naye. Lazima ajaribu kutuliza migawanyiko iliyopo ndani ya Chama cha
Kihafidhina na kukabiliana na uwezekano wa mtikisiko wa kiuchumi.
Changamoto
nyingine kubwa ni pamoja na kuizuia Scotland inayounga mkono Umoja wa
Ulaya dhidi ya kuitisha kura ya uhuru wake ili kubakia katika Umoja wa
Ulaya, na kuimarisha mahusiano mapya ya kibiashara na kidiplomasia ili
kujiandaa kwa hali ya baadaye ya baada ya Brexit.
Waziri wa Afya wa Uingereza, Jeremy
Hunt, amesema anaamini Uingereza sasa imepata Angela Merkel wao:
"Nadhani tunaweza kuhakikisha kuwa nchi hii inapendeza zaidi,
inasisimua, na yenye uchumi wa kijasiriamali katika ulaya nzima.
Itachukua miaka kadhaa kutimiza hilo lakini tuna changamoto kubwa katika
miaka michache ijayo wakati tukitafuta mikataba mipya ya biashara, na
nadhani katika baraza la mawaziri jana hisia zilikuwa ni tumempata Angela Merkel wetu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment