Waziri Mkuu wa Italia,MATTEO RENZI,ametembelea eneo ambako treni mbili za abiria zimegongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 27 na wengine wamejeruhiwa baadhi yao hali zao ni mbaya.
Waziri Mkuu RENZI amewahimiza wananchi wa Italia kutoa damu kuwasaidia majeruhi wa ajali hiyo.
Waziri Mkuu huyo wa Italia ameagiza maafisa wa nchi hiyo kuchunguza kubaini nini chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo.
Treni hizo zilikuwa kwenye njia
moja kati ya Miji ya Bari na Barletta na haijafahamika nini
kilisababisha ajali hiyo wakati hali ya hewa ilikuwa nzuri katika Mkoa
mzima wa Puglia.
Waokoaji kutoka Idara ya Dharura walifika na kuwaokoa abria kutoka kwenye mabehewa yaliyojikunja na kuharibika vibaya na kufanikiwa kumtoa mtoto mchanga akiwa hai na kukimbizwa hospitali.
Home
Kimataifa
Slider
Waziri Mkuu wa Italia atembelea eneo ambako treni mbili za abiria zimegongana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)




0 comments:
Post a Comment