SHIRIKA la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kaunzia Julai 30 mwaka huu kuwa ni mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa abiria badala yake zitatumika kadi.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu matumizi ya kadi
badala ya tiketi.
" Tiketi zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwassa.
Alisema Udart imepunguza
bei ya kadi hizo kutoka sh.4500 ya awali hadi kufikia sh.2000 ili kutoa
fursa kwa kila mwananchi wa kuweza kuipata kadi hizo na kuzitumia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment