Ujenzi
wa kivuko kipya cha Mv Pangani uko katika hatua za mwisho na
kinategemea kumamilika Julai mwaka huu na kuanza kutoa huduma.
Hayo
yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mhandisi. Lekujan Manase alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa
kivuko hicho ambao upo mbioni kukamilika kwa kuanza kutoa huduma kwa
wananchi.
“Kivuko hiki kipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake na
leo tumekuja hapa kukagua mitambo ya kuendeshea kivuko (propulsion
units) pamoja na injini zilizofungwa katika kivuko hiki ili kukamilisha
ujenzi wake na hatimaye kianze kufanya kazi” alisema Mhandisi Manase.
Kwa
upande wake Mkurugenzi kutoka Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme kutoka
Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Dkt. William Nshama
alieleza kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kivuko hicho unaofanywa
kwa kiwango cha kimataifa na kuwa kivuko cha Mv Pangani kinatarajiwa
kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni Mkoani Tanga baada ya ujenzi wake
kukamilika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment