Umoja
wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la
Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa
mkutano huo.
Akiwa katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu
Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika
mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi
wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.
“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa
ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama
Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote
sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema
na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.
Aliongeza kuwa
wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya
kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama
hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.
Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.
Juzi,
BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano
wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman
Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa
CCM.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment