Image
Image

Baraza la wazee CUF lapinga Lipumba na wenzake kusimamishwa uanachama.

Siku moja baada ya tangazo la kusimamishwa uanachama wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Prof Ibrahimu Haruna Lipumba na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, jumuiya ya wazee wa chama  wamepinga uamuzi huo na kusema kuwa maamuzi hayo yamefanyika baada ya ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama hicho uliofanywa na katibu mkuu wa CUF.
Licha ya kutoa msimamo huo jumuiya hiyo ya wazee pia imepeleka malalamiko hayo ya ukiukwaji wa katiba ya chama hicho kwa msajili wa vyama vya siasa na kumtaka msajili huyo kutenda haki kwani wao wanaamini  maamuzi yaliyofanywa na baraza  kuu la CUF yamefanyika kwa lengo la kuzidi kukidhoofisha chama hicho.
Taarifa kutoka ofisi ya makao makuu ya CUF Dar es Salaam inasema maamuzi hayo yamefanyika wakati muafaka lengo ikiwa ni kuhakikisha chama kinarejesha heshima na hadhi yake na kwamba hatua za kuwaondoa itaendelea kwa mwanachama yeyote atakayebainika kukiuka katiba ya chama hicho.
Lakini kwa wanachama wa CUF bado kumeendelea kuwepo migawanyiko ya kimawazo kati ya pande zinazounga mkono maamuzi ya baraza kuu la CUF na wale ambao bado wanaamini kutimuliwa kwa viongozi hao ni ukiukwaji wa katiba ya chama hicho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment