Chama
Cha Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho
upande wa Bara, Magdalena Sakaya.
Uamuzi huo umetolewa jana na Baraza
Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake visiwani Zanzibar kwa lengo
la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo vigogo hao. Sakaya amevuliwa
nyadhifa zote ndani ya chama kabla ya kusimamishwa.
Taarifa kutoka
ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa Baraza hilo limewaadhibu wanachama
15 wakiwemo Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.
Mbali na vigogo
hao, wengine waliopigwa rungu na Baraza Kuu la CUF ni pamoja na Katibu
wa Baraza la Wazee, Shashi Lugeye, Thomas Malima na Naibu Mkurugenzi wa
Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya.
Aidha, Baraza hilo
limemsimamisha uanachama Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma. Hatua
hii inaweka matatani ubunge wa Sakaya na Nachuma kwani wakifikia hatua
ya kufukuzwa watakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Lipumba na
Sakaya hawakupata nafasi ya kujitetea kutokana na kutohudhuria mkutano
huo wakati Shashi alipata nafasi ya kujitetea kutokana na uwepo wake
lakini utetezi wake haukuzaa matunda. Katiba ya chama hicho haiwapi
nafasi wabunge hao kukata rufaa kutokana na uamuzi wa Baraza hilo.
Uamuzi
huo umekuja ikiwa ni siku chacha baada ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama
hicho uliolenga kumchagua Mwenyekiti Mpya kuvunjika kutokana na kuwepo
vurugu kubwa baada ya Profesa Lipumba kuingia ndani ya ukumbi huo na
wafuasi wake wakitaka barua yake ya kutaka kurejea kwenye nafasi yake
ijadiliwe na kukubaliwa.
Hata hivyo, kura zilizopigwa na wajumbe wote
zaidi ya 800, ni kura 14 pekee zilizotaka Profesa Lipumba aendelee na
nafasi ya uenyekiti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment