CHADEMA
inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni
likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha
Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.
Tunaomba umma
upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na
waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni
UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.
Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .
Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.
Imetolewa na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment