Nchini
Libya, Bunge la Libya lenye makao yake mjini Tobruk, lililokutana
Jumatatu hii, Agosti 22, limepiga kura ya kutokua na imani na serikali
ya umoja wa kitaifa (GNA), yenye makao yake mjini Tripoli na ambayo
inaungwa mono na jumuiya ya kimataifa.
Pamoja na kura hii, Bunge limetoa wito kwa Baraza la Kirais kunda haraka serikali mpya.
Tangu
Machi 29, tarehe ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini
Libya (GNA) kufuatia makubaliano ya kisaiasa baina ya wadau wote nchini
Libya yaliyosainiwa nchini Morocco na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa
Desemba 2015, ni mara ya kwanza Bunge, lenye makao yake mjini Tobruk,
mashariki mwa Libya, kufanikiwa kukamilisha idadi ya wabunge
inayohitajika kwa kuweza kukutana. Na hali hii ndio ilipelekea kura hii
kupigwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu na Bunge, wabunge
101 walishiriki kikao hicho, kwa jumla ya wabunge 198. Aguila Saleh,
Spika wa Bunge hilo mapoja na wabunge 61 walipiga kura dhidi ya serikali
ya umoja wa kitaifaTripoli, mbunge mmoja alipiga kura katika neema ya
serikali hiyo na wabunge 39 walijizuia kupiga kura.
Wabunge wengi
wanaamini kwamba serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) imeshindwa
kutekeleza wajibu wake. Imenyesha "kutokuwa na uwezo wa kuongoza nchi,"
Mbunge Rida Omran amesema, kanla ya kuongeza kwamba serikali hii,
"ambayo ni dhaifu toka iundwe," tayari imepoteza maafisa wake wanne.
Bunge
limeomba Baraza la kirais, taasisi yenye wajumbe wanne, kuunda ndani ya
siku kumi na tano, serikali mpya ya dharura itakayoundwa na mawaziri
kati ya 8 na 12. Wakati huo huo, Bunge limesema kuwa maamuzi yote
yaliyopitishwa na Baraza la kirais yanachukuliwa kama "batili".
Kwa
mujibu wa tangazo la kikatiba lililotokana na makubaliano ya kisiasa ya
Desemba 2015, Bunge lina kauli ya mwisho kwa kuonyesha imani yake kwa
serikali.
Home
Kimataifa
Slider
Bunge la Libya lapiga kura ya kutokua na imani na serikali ya umoja wa Kitaifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment