Image
Image

Kenya yasema haipo tayari kushuhudia tena machafuko nchini humo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani CORD na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, wamesema Kenya haitashuhudia tena machafuko baada ya uchaguzi kama ilivyokuwa 2007.
Viongozi hao wamesisitiza kuwa watashindana kwa sera kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Rais Kenyatta na Odinga walikutana kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii wakati wa kumbukumbu ya miaka 38 tangu kufariki kwa rais wa kwanza wa nchi hiyo Jomo Kenyatta.
Odinga naye amesema Kenya ni muhimu kumshinda mtu yeyeote nchini humo mwenye nia ya kuanzisha vurugu.
Viongozi hawa wamekutana baada ya miaka tisa tangu vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya zilizoua zaidi ya watu 1000 na kuwakosesha makaazi zaidi ya watu 60,000 kutokea. Mpaka sasa suali ambalo limekua likiulizwa ni ikiwa kweli Wakenya walijifunza ubaya wa siasa za ukabila.
Kiongozi wa muungano wa upinzani wa CORD, Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni mtoto wa rais wa kwanza wa taifa la Kenya, hayati Mzee Jomo Kenyatta, wanaongoza kambi mbili za upinzani.
Viongozi hawa wanaotokea makabila tofauti, huku Uhuru Kenyata akitokea Kabila la Kikuyu na Raila Odinga akiwa wa Kabila la Luo. Nchini Kenya mabisano yalikua yakiendelea, hasa baada ya upinzani kudai kujiuzulu kwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi IEBC. Mabishano ya uchaguzi wa mwaka 2007 yalisababisha mauaji ya watu zaidi ya 1,200 na kuacha wengine mamia bila ya makaazi.
Mmoja wa wanaharakati aliyesaidia kutuliza ghasia mara baada ya machafuko ya uchaguzi wa mwaka 2007, Mzalendo Kibunjia, alikua akisema bila ya kuongeza hisia katika historia ya chaguzi nchini Kenya, watu wa Kabila la Kikuyu na Waluo wamekuwa katika ushindani kila wakati wa uchaguzi unapofikia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment