Mji
mkuu wa kiuchumi wa Afrika Kusini Johannesburg unashikiliwa kwa sasa na
upinzani, licha ya chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC kuchukua
nafasi ya kwanza katika uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini hakikuweza
kupata wingi wa wajumbe wanaohitajika.
Katika hali ya kukiangusha
chama cha ANC, Jumatatu hii usiku, upinzani uliamua kumuunga mkono
mgombea mmoja katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini humo. Kutokana
na hali hiyo Herman Mashaba amechaguliwa kuwa Meya wa mji mkuu wa
kibiashara wa Afrika Kusini .
Karibu vyama vyote vya upinzani
vilimpiga kura Herman Mashaba. Kwa jumla vyama sita vya upinzani
viliamua kumuunga mkono mgombea huyo ili kuzuia mgombea wa chama tawala
cha ANC. chama tawala, hata hivyo, kiliibuka mshindi katika uchaguzi wa
madiwani mjini Johannesburg, lakini alishindwa kupata washirika ili
kufikia 50% ya kura zilizokua zinahitajika.
Hata chama chenye msimamo
mkali cha Julius Malema, ambacho hata hivyo kilikua kimejizuia kumpigia
kura mgombea wa upinzani, kiliamua kumuunga mkono ili kukiangusha chama
cha ANC.
Herman Mashaba ameahidi mabadiliko na kutoa kipaumbele kwa
ajira. "Tutafanya mabadiliko ambayo yataleta ajira, kwa jumla ya wakazi
800, mtu 1 kati ya 3, hana ajira. Tunapaswa kukabiliana na tatizo hili,
na kuna haja ya kuharakia kutafutia ufumbuzi wa tatizo hilo", amedema Bw
Mashaba.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment