Mratibu
wa mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Edem
Kodjo, ametangaza kuanza kwa zoezi la maandalizi ya kamati ya mazungumzo
Jumanne hii asubuhi katika mji wa Kinshasa.
Katika shughuli hizi,
jopo la wanasiasa na wanaharakati wa asasi za kiraia watachagua hasa
sehemu ambapo mikutano hii itafanyika, watu wanaopaswa kushiriki na
lengo linalotafutwa.
Hata hivyo upinzani nchini DRC unaonekana
kugawanyika kati ya wale ambao wanataka kushiriki mazungumzo bila
masharti na wale wanaotoa masharti kabla ya kushiriki.
Chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba kimekataa katu katu wazo lolote la kufanya mazungumzo na serikali ilioko madarakani.
Muungano
wa vyama vya upinzani unaoundwa na Etienne Tshisekedi na Moise Katumbi
unakubaliana juu ya kanuni ya mazungumzo na umetoa masharti ya kushiriki
mazungumzo hayo.
Muungano huo umeomba kuachiwa huru wale unaowachukulia kama wafungwa wa kisiasa.
rais Joseph Kabila amewaachia huru baadhi yao. Lakini muungano wa vyaa vya upinzani wa "Rassemblement" umesema idadi haitoshi.
Pia muungano huo unaomba Edem Kodjo, kuachia ngazi, kwani anaegemea upande wa serikali.
Edem Kodjo hivi karibuni aliungwa mkono na serikali ya Congo pamoja na Kanisa Katoliki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment