JESHI la Polisi limejipanga kukabiliana na Operesheni Ukuta, huku viongozi mbalimbali wa Chadema wakikamatwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Simon Sirro, alisema kwamba maandamano hayo hayatafanyika na
jeshi la polisi limejipanga kuyazuia maandamano hayo.
Kamanda Sirro
alisema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayethubutu kuingia
barabarani kutokana na jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi
wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.
Alisema utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa, hivyo kufanya bila kufuata utaratibu hakutaruhusiwa.
Kamishna
Sirro alisema watu wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja amani
hawatakuwa na nafasi na kwamba watadhibitiwa na jeshi hilo.
BUKOBA
Taharuki
kubwa imejitokeza jana katika Manispaa ya Bukoba kufuatia milipuko
mikubwa ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU).
Milipuko hiyo ya mabomu ilianza kusikika saa nne asubuhi maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi, alisema kuwa wapo katika mazoezi ya kawaida.
VIONGOZI WAKAMATWA
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita, Upendo Peneza (Chadema) pamoja na Ofisa
wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Tungaraza Njugu, wamekamatwa jana
wilayani Bukombe mkoani Geita.
Viongozi hao wamekamatwa wakati wakiwa
kwenye vikao vya chama pamoja na wanachama wengine 12, wakituhumiwa
kupanga maandamano ya Ukuta.
Katika maeneo mbalimbali ya nchi hivi
sasa, askari polisi wamekuwa wakiendesha mazoezi yenye lengo la
kujipanga kukabiliana na Ukuta.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment