Nchi
ya Urusi, juma hili itajua hatma yake ikiwa wanamichezo wake wenye
ulemavu wataruhusiwa kushiriki kwenye michezo ya Paralympic mjini Rio,
Brazil, itakayoanza mwezi ujao.
Mahakama ya kimataifa ya michezo,
Cas, inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu rufaa iliyokatwa na nchi ya Urusi,
ikipinga uamuzi wa kamati ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu iliyowazuia
wanamichezo wake wote kushiriki michezo ijayo.
Shirikisho la kamati
ya olimpiki kwa watu wenye ulemavu IPC, lilichukua uamuzik wa kuwafungia
wanamichezo wote wa Urusi, baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya McLaren
iliyoonesha usaidizi wa Serikali kuwafanya wanariadha wake wasichukuliwe
vipimo kubaini ikiwa wanatumia dawa za kusisimua misuli au la.
Michezo ya olimpiki kwa watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia September 7 mwaka huu.
Uamuzi
wa IPC ulienda sambamba na ule wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki, IOC,
ambayol iliamua baadae kutowafungia kabisa wanamichezo wa Urusi na
baadhik yao waliruhusiwa kushiriki.
Hata hivyo kamati ya kimataifa ya
Olimpiki imejikuta ikikosolewa pakubwa kutokana na kile kinachosemwa
kuwa kamati hiyo ilidharau na kukacha mapendekezo ya shirika la
kimataifa linalosimamia matumizi ya dawa za kusisimua misuli, Wada.
Katika
uamuzi wake, IOC, ilitoa mamlaka kwa mashirikisho mbalimbali ya michezo
kuamua nik wanariadha wapi wa Urusi wataruhusiwa na wale ambao
hawataruhusiwa ambapo baadae kamati ya IOCm ndio ilikuwa mwamuzi wa
mwisho.
Mwisho wa siku zaidi ya wanariadha 270 wa Urusi waliruhusiwa
kushindana kwenye michezo ya Olimpiki iliyomalizika mwishoni mwa juma,
ambapo Urusi ilijinyakulia medali 56 kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment