Kiongozi
wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Aboubakar Shekau amejeruhiwa
vibaya kwenye shambulio la angani lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo,
taarifa ya jeshi imesema.
Makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa.
Taarifa
kutoka kwa jeshi la angani la Nigeria imesema shambulio hilo
lilitekelezwa Ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa
wakishiriki sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale
katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa jeshi, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.
"Kiongozi
wao, anayefahamika kama, "Abubakar Shekau", anaaminika kujeruhiwa
vibaya begani," jeshi limesema kupitia taarifa iliyotolewa na naibu mkuu
wa mawasiliano Kanali Sani Kukasheka Usman.
Kundi la Boko Haram karibuni limekabiliwa na mzozo wa uongozi.
Kundi la Islamic State lilitangaza kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram.
Lakini
muda mfupi baadaye, Shekau alisema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi
hilo na akamshtumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.
Home
Kimataifa
Slider
Kiongozi wa Boko Haram Nigeria, Aboubakar Shekau ajeruhiwa kwenye shambulio nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment