
Na.DevothaSongorwa,Morogoro ................................................................................................................................................................
Wananchi wameaswa kuwa na desturi ya kujitolea kuchangia damu ili kuweza kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu ikiwamo wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
ABRAHAM CHARLES MAHARAGE ambaye ni Mratibu Msaidizi wa damu salama kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro amesema katika zoezi hilo muitikio wa kuchangia damu umekuwa mdogo kutokana na kutotolewa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kuondokana na imasni potofu na hivyo kutambua umuhimu wa kuchangia damu salama.
MAHARAGE amefafanua kwa kina kuwa kitengo cha damu salama kinaendelea kuhamasisha jamii kuchangia damu salama kwa hiari ili kuokoa maisha ya wenye mahitaji..
Wakati huohuo mkazi wa manispaa ya Mororgoro HAME MRISHO KONDO amesema pamoja na kuchangia damu kunasaidia kuokoa maisha ya watu wenye shida ya kuongezewa damu, unapata fursa ya kufahamu afya yako na kujua namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Mkazi wa Kihonda CHRISTINA JUMA ametoa wito wananchi kutembelea vituo vya afya ili kupima afya yao ikiwa ni pamoja na kuzifahamu sifa za kuchangia damu salama na kupunguza vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa damu.
Hata hivyo wakazi hao wamewataka wananchi kuachana na fikra potofu kuwa kuchangia damu ni kuweka maisha yao hatarini, na badala yake wazingatie masharti ya daktari baada ya kuchangia damu ili kuufanya mwili uendelee kuzalisha damu ya kutosha.

0 comments:
Post a Comment